From: xxxxx@tiscali.co.uk>
Sent: Friday, June 10, 2005 4:57 AM
To: waciku@gatua.com>
Subject: kirathimo
Ũngĩrogerera thome wĩ mbũri, ũngĩrotukĩrĩrwo ũkĩgĩrima,
ũngĩroteretha ũkĩinĩ na watua kwarahũka warahũke ũnyitĩte
ithunya. Ũgĩ waku ũrotũguna na ũgune njiarwa ciitũ.
Thaai, thaathaiya thaai!
Wachira,
United Kingdom
From: ndesanjo macha xxxxxxx@yahoo.com>
Sent: Tuesday, June 14, 2005 10:17 AM
To: Gatua wa Mbugwa waciku@gatua.com>
Subject: Re: Asante Ndugu
Ndugu yangu Gatua,
Asante sana kwa waraka wako. Nimefurahi sana kuupata.
Mimi nilikuwa nimepanga kuwa nitakuandikia hivi karibuni.
Nilifurahi mno kusikia kuwa kuna mshairi anatengeneza CD
za mashairi kwa lugha za Kiafrika. Hongera sana kwa kazi hiyo
kubwa. Mimi nami ni mshairi, hasa wa kiswahili. Mashairi huru
(bila kujali vina na mizani!).
Ukiwa na habari yoyote au kazi mpya usisite kunipa taarifa ili
niweke kwenye blogu.
Ningependa sana siku moja tufanye mahojiano. Blogu yangu
inasomwa na watu wengi wanaojali lugha za Kiafrika
(na pia wakenya wengi) kwa kuwa moja ya sababu za kuianzisha
ni kujaribu kusafisha fikra zetu na kukomboa akili zetu.
Ningefurahi sana kama tungehojiana juu ya kazi zako, mipango
ya baadaye, watu wanavyopokea kazi zako, ushairi wa kiafrika,
na mambo kama hayo.
Basi tuendelee kuwasiliana.
Uhuru!
Nduguyo ndesanjo,
Duniani
From: mshairi xxxxx@blogger.com>
To: xxxxx@yahoo.com>
Sent: Tuesday, June 14, 2005 10:32 AM
Subject: Mmoja wa wasomaji akizungumzia mashairi yako
Asante Ndesanjo ndugu yangu. Mashairi ya mshairi huyu
(Gatua wa Mbũgwa) yanapendeza sana (tena yanilazimisha
kujifunza Gĩkũyũ haraka sana = 'crash course'
Msomaji wa blogu ya Ndesanjo,
Duniani